Jinsi ya Kupata Kibali cha Ujenzi
Habari za wakati mpendwa msomaji! hivi kwa kawaida ni watu wangapi ambao wanafikiria kujenga? hapana shaka ukifanya utafiti utakuta kila binadamu mwenye akili timamu anafikiria kujenga. Hivyo basi twende pamoja katika habari hii muhimu kwako.
Hatua za kufuata ili kupewa kibali cha kujenga jengo.
Kwanza kabisa wanaotoa kibali cha kuruhusu jengo lijengwe ni mamlaka za kiserikali za eneo husika hasa manispaa, kwa maana wao wanao ramani ya mji mzima inayoonesha mipangilio ya aina za majengo yanayotakiwa kujengwa katika kila mtaa.
1. Hati halali ya eneo – Hii hasa kwa wale wanaotaka kujenga majengo ya gholofa na ya kibiashara ni lazima kuhakikisha unakuwa na hati halali inayoonesha kwamba sehemu unayotaka kujenga ni mali yako.
2. Michoro kamili na iliyowekwa muhuri – hii ni ile ya msanifu majengo(architectural drawings) kwa majengo ya kawaida ya kuishi(residential) ya chini (one storey) kwa yale ya ghorofa pia itahitajika michoro ya mhandisi majengo(structural drawings), mhandisi umeme (electrical drawings), na michoro ya mfumo wa maji safi na taka (plumbing).
Kumbuka : michoro hii yote inatakiwa iwe imepigwa muhuri ili kuonesha kwamba imechorwa na wataalamu wenye sifa na wanaotambulika.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: omarisaidi77@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 629218, +255 689636501,
Karibu Sana!!!
Ni safi sana kuona taarifa muhimu kwa wanao elewa na wasio elewa mimi lia ni muhanga nilijenga bila kubali kwa kutokujua so mimi naanza wapi kuanza kufuatilia?
ReplyDelete